KIUNGO MGUMU AREJEA NA KUANZA KAZI SIMBA

ULE uwezo uliopo kwenye miguu ya kiungo mgumu wa Simba, Sadio Kanoute uliwazubaza Waarabu wa Morocco, Wydad Casablanca kutokana na balaa aliloonyesha.

Ikumbukwe kwamba Kanoute alirejea na kuanza kikosi cha kwanza licha ya kukosekana kwenye mechi nne mfululizo ikiwa ni pamoja na mchezo dhidi ya Yanga.

Alikosekana mchezo dhidi ya Raja Casablanca hatua ya makundi, Ihefu mechi ya Kombe la Shirikisho na ligi pamoja na Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga na kumfanya awe jukwaani dakika 360 za ushindani.

Alikiwasha Aprili 22 ubao wa Uwanja wa Mkapa uliposoma Simba 1-0 Wydad mtupiaji akiwa ni Jean Baleke aliyetumia pasi ya Kibu Dennis.

Kanoute ambaye ametoka kupona maumivu ya nyonga aliyeyusha dakika 90 mazima huku mikato yake ya kimyakimya alitembeza dakika ya 12 alichezewa faulo dakika ya 4 huku akiokoa hatari dakika ya 4.

Kiungo huyo alipiga mashuti mawili ambayo hayakulenga lango ilikuwa dakika ya 31 na 36 alifanya kazi kubwa kwenye eneo la ukabaji akishirikiana na mzawa Mzamiru Yassin.

Yupo kwenye kikosi ambacho kimewasili Morocco leo Aprili 26 kwa ajili ya kete ya pili dhidi ya Wydad Aprili 28,2023 Uwanja wa Mohamed V.