MSHAMBULIAJI wa Manchester City Erling Haaland yuko njiani kutengeneza rekodi zake binafsi bora zaidi katika historia ya Premier League.
Haaland ana umri wa miaka 22 tu na tayari amezoea ligi na nchi mpya kwa haraka sana sasa anafurahia msimu wake wa kwanza bora akiwa na Man City chini ya Kocha Pep Guardiola. Man City bado wanapigania treble na moto wa Haaland umekuwa ukiwachoma sana wapinzani wao.
Nyota huyo wa kimataifa wa Norway tayari amefikia rekodi ya Mohamed Salah ya kufunga mabao 32 katika mechi 38 za Premier.
Kwa sasa anahitaji tatu zaidi kuvunja rekodi zote za Premier zilizowekwa na Andy Cole (1993-94) na Alan Shearer (1994-95) wakati ligi ikipigwa kwa mechi 42.
Lakini pia anaivunja pande zote. Amefunga mabao 12 katika mechi nane za Ligi ya Mabingwa Ulaya ‘UEFA’ na ana mabao 48 katika mashindano yote – ambayo tayari ni rekodi katika Premier.
Man City wamesalia na hadi mechi 13 na ikiwa Haaland anaweza kuendelea na rekodi yake ya kufunga mabao katika kila mechi basi atavunja rekodi kadhaa.
“Nataka, natamani avunje rekodi zote iwezekanavyo kwa sababu akifunga mabao mengi hiyo inamaanisha inatusaidia,” Guardiola aliwaambia wanahabari hivi karibuni na kuongeza:
“Inavutia na bado tuna mechi nane au 10 na anakaribia kuzivunja zote.”
Wakati tunaona kuwa Haaland kwa sasa anakamua, unajua kuhusu wale waliomtangulia kwenye Premier na nini walikifanya?
Hapa kuna takwimu za michuano yote kwa Haaland na kulinganisha dhidi ya mastraika bora walipokuwa kwenye misimu yao bora zaidi mechi za England kuanzia mwaka 1992.
NB: Kwa upande wa mataji hadi sasa Haaland hajafanikiwa kubeba lolote lakini yuko kwenye nafasi ya kubeba matatu, la Premier League, UEFA na Kombe la FA.
ERLING HAALAND (2022-23)
Mechi: 41
Alizoanza: 39
Alizofanyiwa mabadiliko: 2
Mabao: 48
Asisti: 6
Penalti alizofunga: 7
Hat-trick: 7
Bao la free-kick: 0
Bao kwa dakika: 66
Dakika bila bao la penalti: 77
Bao/asisti kwa dakika: 58
Mataji aliyoshinda: (msimu haujaisha)
MOHAMED SALAH (2017-18)
Mechi: 52
Alizoanza:
Alizofanyiwa mabadiliko:
Mabao: 44
Asisti: 16
Penalti alizofunga: 1
Hat-trick: 1
Bao la free-kick: 0
Bao kwa dakika: 93
Dakika bila bao la penalti: 95
Bao/asisti kwa dakika: 68
Mataji aliyoshinda: Hakuna
LUIS SUAREZ (2013-14)
Mechi: 37
Alizoanza: 36
Alizofanyiwa mabadiliko: 1
Mabao: 31
Asisti: 19
Penalti alizofunga: 0
Hat-trick: 2
Bao la free-kick: 3
Bao kwa dakika: 105
Dakika bila bao la penalti: 105
Bao/asisti kwa dakika: 64
Mataji aliyoshinda: Hakuna
CRISTIANO RONALDO (2007-08)
Mechi: 49
Alizoanza: 46
Alizofanyiwa mabadiliko: 3
Mabao: 42
Asisti: 8
Penalti alizofunga: 6
Hat-trick: 1
Mabao ya free-kick: 5
Bao kwa dakika: 99
Dakika bila bao la penalti: 115
Bao/asisti kwa dakika: 83
Mataji aliyoshinda: Ngao ya Jamii, Premier League, Champions League