Skip to content
UKIWA ni mchezo wa kwanza hatua ya robo fainali Kombe la Shirikisho, ushindi unarejeja Tanzania.
Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Godswill Akpabio huko Nigeria umesoma Rivers United 0-2 Yanga.
Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ilipata ushindi huo kwa mabao ya nyota Fiston Mayele.
Mayele alipachika mabao hayo kipindi cha pili ilikuwa dakika ya 71 na 82 kweye mchezo huo uliokuwa ni wa kasi mwanzo mwisho.
Shukrani kwa Bakari Mwamnyeto mzawa ambaye ametoa pasi zote mbili kwenye mchezo wa leo ugenini.
Kete ya pili Yanga watakuwa nyumbani wanahitaji kulinda ushindi huo na kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.