SIMBA YAIBUKA NA USHINDI DHIDI YA WYDAD

KIWA Uwanja wa Mkapà klabu ya Simba imepata ushindi wa bao 1-0 Wydad Casablanca.

Huu ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali na bao limefungwa na Jean Baleke dakika ya 30.

Licha ya kuwa na mabadiliko katika kikosi cha kwanza akianza Ally Salim langoni bado walikuwa na kushinda mchezo huo.

Baleke alikwama kukamilisha dakika 90 na nafasi yake ilichukuliwa na nahodha John Bocco kwenye mchezo huo.

Kazi inaanza kwa Simba ambayo ingekuwa na utulivu leo ingepata ushindi wa mabao zaidi ya mawili.