UBAO wa Uwanja wa Mkapa unasoma Simba 1-0 Wydad Casablanca ikiwa ni hatua ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Bao la kuongoza limefungwa na mshambuliaji Jean Baleke akiwa ndani ya 18 dakika ya 30.
Dakika 45 za mwanzo Simba imepata umiliki wa asilimia 55 huku Wydad wakiwa na umiliki wa asilimia 45.
Ushindani ni mkubwa huku Wydad wao wakicheza kwa kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza.
Kipa namba tatu wa Simba Ally Salim yupo langoni kwenye mchezo huu wa leo huku benchi akiwa ni Beno Kakolanya ambaye ni kipa namba mbili.