CITY YATINGA NUSU FAINALI UEFA

MANCHESTER City inatinga hatua ya nusu fainali UEFA Champions League kwa jumla ya ushindi wa mabao 1-4.

Katika mchezo wa robo fainali uliochezwa Allianz Arena ubao ulisoma Bayern Munich 1-1 City.

City ilianza kupata ushindi kupitia kwa Erling Haaland dakika ya 57.

Ni Joshua Kimmich dakika ya 83 alipachika bao katika mchezo huo kwa pigo la penalti.

Mashuti 19 Bayern Munich walipiga huku City ilipiga mashuti 7 ndani ya dakika 90.