Home Uncategorized MAYELE MTU WA KAZIKAZI, KAMBEBA SALIM

MAYELE MTU WA KAZIKAZI, KAMBEBA SALIM

FISTON Mayele moja ya washambuliaji wenye akili na wanalijua lango dhidi ya Simba Aprili 16 anashikilia rekodi ya kupiga mashuti mengi yaliyolenga lango.

Ni ubora wake kwenye kutafuta kufunga kumemfanya kipa wa Simba aonekane ni bora kutokana na kuwa makini kwenye kuokoa hatari hizo.

Ingekuwa angekwama kuokoa hatari alizopigiwa na Mayele ingekuwa ni habari nyingine kwa upande wa Simba baada ya dakika 90.

Ally Salim umakini wake katika kuokoa hatari ulikuwa chini labda tuseme mipira ilikuwa inateleza asilimia 70 ya kona walizopata Yanga zimetokana na kutema kwake mipira ambayo tayari ilikuwa katika himaya yake.

Miongoni mwa mipira ambayo aliitema ilikuwa ni dakika ya 12,15 na hata uokoaji wake wa kona bado ulikuwa unagotea ndani ya 18 na mabeki wakaweka usawa kwenye kukamilisha majukumu yao.

Khalid Aucho kiungo wa kazi na Mayele walikutana na Onyango ambaye alikuwa na siku nzuri kazini jambo lililofanya Yanga wakakwama kupata ushindi.

Salim bado ana muda wa kujifunza kuwa bora zaidi haina maana kuokoa hatari dhidi ya Yanga kazi imekwisha ana kazi ya kurejea darasani na kujifunza zaidi na zaidi ili awe bora zaidi.

Kukosa kwake mechi za mara kwa mara kunamfanya awe hapo alipo na anaweza kuondoka na kuwa imara zaidi ikiwa atajifunza.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amebainisha kuwa moja ya makipa wazuri na bora ndani ya ardhi ya Bongo ni pamoja na Salim.

“Ukianza kuwataja makipa bora Tanzania, moja Aishi Manula mbili ni Beno Kakolanya na tatu ni Ally Salim,”.

Previous articleVIDEO:JEMBE AMVAA KOCHA YANGA/SIMBA KUBEBWA
Next articleSHINDA TSH MILIONI 90,000,000/= ZA MERIDIANBET KILA SIKU