KAGERA SUGAR KUREJEA WAKIWA IMARA

MECKY Maxime, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa waterejea kwenye mechi zilizobaki wakiwa imara kwa kupata matokeo chanya.

Timu hiyo haina bahati dhidi ya Yanga msimu huu wa 2022/23 kwa kufungwa nje ndani mchezo wa kwanza ilitunguliwa bao 0-1 na ule mzunguko wa pili ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Yanga 5-0 Kagera Sugar.

Maxime amesema kuwa wanatambua walikwama kushinda mchezo uliopita jambo linalowapa nguvu kujipanga kwa mechi zinazofuata.

“Hatukuwa na siku nzuri dhidi ya Yanga ule ulikuwa mtego kwetu nasi tukaingia hivyo kwa sasa ambacho tunakifanya ni kujipanga kuwa imara kwa mechi zinazofuata.

“Hakuna namna bado wachezaji wanajuhudi na uwezo wao ni mkubwa ndio maana wanashiriki ligi kwa makosa waliyofanya tutafanyia kazi ili tupate matokeo kwani mpira ni mbinu na wakati mwingine huwa unakuwa na matokeo tofauti,” alisema.

Mchezo ujao wa Kagera Sugar unatarajiwa kuchezwa Aprili 23 dhidi ya Mbeya City, Uwanja wa Kaitaba.