ALLY SALIM BADO SANA KUWA BORA

ALLY Salim kipa namba tatu wa Simba mchezo wake wa kwanza akiwa langoni dhidi ya Yanga amefanikiwa kukamilisha dakika 90 bila kufungwa.

Bado anajitafuta kutokana na makosa mengi ya kiufundi hasa kwenye kuokoa na kutema hapo ndipo panamfanya awe kwenye kazi ngumu ya kufanya.

Ally amesababisha kona nne kwenye mchezo dhidi ya Yanga kutokana na makosa ambayo amefanya wakati wa kuokoa mpira.

Ili awe bora ni lazima aongeze kazi kubwa kwenye kuokoa hatari langoni mwake ili awe imara.

Bado safari ni ndefu kwa Ally kufikia uimara kama ilivyo Aishi Manula, Djigui Diarra na Beno Kakolanya.

Aprili 16 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 2-0 Yanga huku mabao yakifungwa na Henock Inonga na Kibu Dennis.