SIMBA:NJOONI MUMUONE CHAMA

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa leo Uwanja wa Mkapa watamuona Clatous Chama waliyemzoea kwenye mechi za kimataifa.

Chama amekuwa akipeta kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa akiwa na hat trick moja dhidi ya Horoya alipofunga mabao matatu lakini hajawahi kuwatungua watani zao wa jadi Yanga.

Katika mchezo uliopita wa mzunguko wa kwanza Oktoba 23 ubao wa Uwanja wa Mkapa uliposoma Yanga 1-1 Simba, Chama alitoa pasi moja ya bao kwa Agustino Okra lakini hakufunga.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa watamuona Chama mwenyewe Jumapili kutokana na maandalizi bora.

“Wengi wanasema Chama huwa hawamuoni kwenye mechi dhidi ya Yanga wanasahau kwamba wapinzani wanapofika uwanjani huwa wanaanza kumshangaa na kumchezea kwa fujo jambo ambalo hajazoea.

“Ikiwa anafanya makubwa kwenye mechi kubwa za kimataifa anaweza asionekane kwenye mchezo wa wapinzani wetu kutoka hapo Jangwani? Hivyo basi Jumapili mtamuona Chama mwenyewe yuleyule anayependa kucheza mpira kwa nafasi,” .