NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amemkimbiza kinomanoma Roberto Oliveira raia wa Brazil kwenye upande wa kusepa na pointi tatu muhimu ndani ya dakika 450.
Katika mechi tano za hivi karibuni Yanga haikuwa na namna ilisepa na pointi zote 15 ilizokuwa inasaka huku Oliveira akikwama kufanikisha jambo hilo.
Simba kwenye msako wa pointi 15 imegotea kwenye pointi 13 ikiyeyusha pointi mbili kwa kuwa ilishinda mechi nne na kuambulia sare moja.
Upande wa utupiaji Simba ilitupia mabao10 kibindoni kwenye mechi tano huku wao wakitunguliwa mabao mawilina wapinzani wao.
Ile ya Yanga kwa upande wa ushambuliaji ilitupia mabao 12 kwenye ulinzi waliokota bao moja pekee
Hizi hapa za Simba:-Ihefu -2 Simba, Mtibwa 0-3 Simba,Simba 1-1 Azam FC,Simba 3-1 Singida Big Stars,Dodoma Jiji 0-1 Simba.
Hizi za Yanga:-Yanga 5-0Kagera Sugar,Yanga 3-1Geita Gold,Yanga 1-0 KMC,Yanga 2-0 Namungo,Yanga 1-0 Ruvu Shooting.