MZAWA Dickosn Job beki wa kazi ngumu bado yupo ndani ya kikosi cha Yanga baada ya kuongeza dili jipya la kuendelea kuitumikia timu hiyo.
Awali kulikuwa na mvutano mkubwa kwenye upande wa maslahi jambo lililofanya asubiri kwanza kusaini mkataba mpya.
Alikuwa anatajwa kuingia rada za mabosi wa Dar, Azam FC ambao walikuwa wanahitaji saini yake.
Job rasmi ataendelea kuvaa uzi wa Yanga baada ya Aprili 15 kutangazwa kuwa bado ni Mwananchi.
Ni dili la miaka miwili ameongeza nyota huyo ambaye aliibuka hapo akitokea Mtibwa Sugar.