JEAN BALEKE AWALIZA IHEFU, ALLY SALIM MIKONO MIA
LICHA ya Ihefu kuwa bora kwenye mchezo wa leo mbele ya Simba kwenye upande wa umiliki wamekwama kusepa na pointi tatu. Dakika 90 zimekamilika ubao wa Uwanja wa Highland Estate unasoma Ihefu 0-2 Simba. Mabao yote mawili yamefungwa na Jean Baleke kipindi cha pili katika dakika za lala salama ilikuwa dakika ya 83 na 86….