CHELSEA wanapita kwenye kipindi kigumu huku wakiwa wanalipa mshahara mkubwa wachezaji wao.
Hadi sasa wameondolewa kwenye mashindano yote mawili ya vikombe vya nyumbani.
WANALIPA MISHAHARA MIKUBWA
Chelsea ndio klabu ya pili kwa Premier League ambayo inalipa mishahara mikubwa kwa mwaka, wakitanguliwa na Manchester United.
Kwa mujibu wa mtandao ambao unahusika na mishahara ya klabu za ligi kubwa Ulaya, inadaiwa kuwa Chelsea kila mwaka inalipa zaidi ya pauni mil 169.7 kwa wachezaji wao wote wa kikosi cha kwanza.
Manchester United ambao ndio vinara kwa Premier wao wanalipa kila mwaka pauni mil 222.9, wakati Man City wakishika nafasi ya tatu wakilipa pauni mil 163.
Liverpool wako nafasi ya nne wakilipa pauni mil 141.7, Tottenham wa tano wakikamuliwa pauni mil 101.3 na Arsenal wa sita bajeti yao ya mishahara ikiwa pauni mil 85.4 kwa mwaka.
USAJILI GHALI ZAIDI ULAYA
Kwa ujumla klabu za Premier zilitumia kama pauni mil 780 kwa usajili wa wachezaji 52 kwenye dirisha dogo msimu huu, hiyo ni kwa mujibu wa kituo cha Sky.
Wamezidi ligi zingine bora Ulaya Ligue 1, Bundesliga, Serie A na La Liga zote kwa pamoja.
Huku klabu zikiuza wachezaji kwa pauni mil 105 na kufanya Premier itumie pauni mil 675 kwenye usajili wa majira ya baridi.
Chelsea ilivunja rekodi ya usajili kwa Uingereza wakitumia pauni mil 106.8 kumsajili kiungo Enzo Fernandez, 22, kutoka Benfica dakika za mwisho.
Mchezaji wa pili ghali pia alitua Chelsea kwa pauni mil 88 ambaye ni winga Mykhailo Mudryk kutoka Shakhtar Donetsk.
Hii iliwafanya Chelsea kuwa ndio klabu iliyotumia mkwanja mrefu zaidi usajili wa Januari kwani kwa ujumla waliweka mezani pauni mil 323 kusajili wachezaji wapya nane.
Wengine waliosajiliwa ni beki Benoit Badiashile alitua kwa pauni mil 35, straika wa PSV, Noni Madueke aliikamua pauni mil 29 pia Chelsea wakatoa pauni mil 26 kwa beki wa pembeni mwenye miaka 19, Malo Gusto kutoka Lyon.
Mbali na hao kuna pauni mil 18 zilizotumika kumshusha Andrey Santos kutoka Vasco de Gama na David Datro Fofana akatua kwa pauni mil 8 kutoka Molde usisahau Todd Boehly akamchukua kwa mkopo Joao Felix kutoka Atletico Madrid kwa ada ya pauni mil 10. Mchezaji pekee ambaye walimuuza ni Jorginho aliyeenda Arsenal kwa euro mil 11.3.
Hapa kuna listi ya wachezaji wa Chelsea na mishahara yao ambayo ni ya wiki na kwa mwaka msimu huu huku Raheem Sterling akiongoza jahazi.