UONGOZI wa Yanga umebainisha kuwa kwenye hatua ya robo fainali watafanya kweli kama ilivyokuwa katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Imemaliza mwendo hatua ya makundi ikiongoza kundi D na kibindoni ina pointi 13 mchezo wake wa mwisho ilikuwa dhidi ya TP Mazembe iliposhinda kwa bao 0-1 ikiwa ugenini
Meneja wa Yanga, Walter Harrison amesema kuwa wanatambua kazi kubwa ilikuwa kwenye hatua ya robo fainali jambo ambalo limefanikiwa kwa kiwango kikubwa.
“Dhamira yetu ilikuwa ni kushinda na kukamilisha hesabu tukiwa tunaongoza kundi kwa hatua ambayo tumefikia sio mbaya tunahitaji kuwa na mwendelezo mzuri kwenye hatua ya robo fainali.
“Mipango ipo vizuri na tunaamini tutaendelea kufanya vizuri kikubwa mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kwani tunaamini mambo mazuri yanakuja,”.
Yanga itacheza na Rivers United kwenye hatua ya robo fainali ambapo wataanzia ugenini kisha kete ya pili itakamilishiwa Uwanja wa Mkapa.
Mshindi kwenye mechi hizo mbili atasepa na tiketi ya kutinga hatua ya nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika.