SINGIDA BIG STARS WAO YANGA AMA GEITA HAINA TATIZO

BAADA ya kufanikiwa kukata tiketi ya kutinga hatua ya nusu fainali Azam Sports Federation Kocha Mkuu wa Singida Big Stars Hans Pluijm amesema kuwa iwe Yanga ama Geita Gold wapo tayari kuwakabili.

Singida Big Stars ilipata ushindi dhidi ya Mbeya City kwa mabao 4-1 mchezo war obo fainali uliochezwa Uwanja wa Liti.

Kocha huyo amebainisha kuwa kazi kubwa ilifanywa na wachezaji wake kusaka ushindi jambo ambalo kila mmoja anafurahia kwa matokeo mazuri.

“Kikubwa ni kwamba tumeshinda na kufika hatua ya nusu fainali hapo ambaye tutakutana naye lazima tupambane naye kwa kuwa tupo tayari kwa ajili ya mchezo huo iwe ni Geita ama Yanga.

“Dakika 90 huwezi kuzizungumzia kwa sasa ni mpaka mchezo utakapokamilikahapo utajua unacheza na yupi. Nina amini kazi bado inaendelea kwenye mechi hizi ambazo zina ushindani mkubwa,”.

Singida Big Stars itakutana na mshindi wa mchezo kati ya Yanga na Geita Gold unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.