WANANCHI MIKONONI MWA RIVERS,WASEPA NA TUZO

YANGA kwenye hatua ya robo fainali Kombe la Shirikisho imepangwa kumenyana na Rivers United.

Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi imefuzu hatua ya robo fainali ikiwa namba moja kwenye kundi D na pointi zake ni 13.

Droo ya hatua ya robo fainali imecezwa nchini Misri Aprili 5 na Yanga kuangukia mikononi mwa Rivers United ya Nigeria.

Wakati hayo yakitokea nyota Mudhathir Yahya bao lake alilofunga kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe limechaguliwa kuwa bao bora hatua ya makundi.

Muda alifunga bao hilo ubao wa Uwanja wa Mkapa uliposoma Yanga 3-1 TP Mazembe.