MWAMBA Anuari Jabir amepata dili a kwenda kufanya majaribio kwa muda wa siku 14 kutoka Klabu ya Ligi Kuu ya Ubelgiji (Pro League Belgium)
Jumatatu ya Aprili 3 aliwasili salama Ubegiji kwa kwa ajili ya majaribio ya kuchezea timu hiyo na mipango ikienda sawa anaweza kumwaga wino huko.
Jabir ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Mecky Maxime ambaye ameweka wazi kuwa wamempa ruhusa kijana wao akatafute changamoto mpya kama mambo yatakwenda sawa.
“Ni kweli tumemruhusu Anuary Jabir kwenye majaribio ya wiki mbili nchini Ubegiji kwenye Klabu ya KAA Gent inayoshiriki ligi ya huko,”.
Wakati mwamba akiibukia Ubelgiji mshikaji wake Makame Bui amepewa mkono wa asante ndani ya timu hiyo baada ya kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba wake.
Zinakuwa ni stori mbili ndani ya Aprili kwa washkaji wa Kagera Sugar ambapo moja ni tamu kwa Jabir huku kwa Makame ikiwa ni chungu.