LEO Azam FC inatupa kete yake kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Azam Complex.
Mshindi ataungana na Singida ig Stars hatua ya nusu fainali kwa kuwa wao walishatangulia baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Mbeya City.
Azam FC ama Mtibwa Sugar kwa atakayepoteza mchezo wa leo atakuwa na dakika nyingine 90 za kulipa kisasi kwenye mchezo wa ligi.
Mchezo wao unaofuata wapinzani hawa kwenye hatua ya robo fainali utakuwa ni wa ligi na utachezwa hapohapo Uwanja wa Azam Complex.
Ni Aprili 8 wababe hao watakuwa na kazi ya kusaka ushindi mwingine tena kwenye mchezo wa mzunguko wa pili.
Miongoni mwa nyota wa Azam FC ambao wapo kwenye maandalizi ya mchezo huo ni pamoja na kiungo James Akamiko, Prince Dube, Idd Suleiman na Sopu.