Home Sports YANGA NI NAMBA MOJA SHIRIKISHO AFRIKA

YANGA NI NAMBA MOJA SHIRIKISHO AFRIKA

YANGA ni vinara wa kundi D katika Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ubao wa Uwanja wa TP Mazembe kusoma TP Mazembe 0-1 Yanga.

Bao la ushindi ni mali ya Farid Mussa huku kipa Metacha Mnata ikiwa ni mchezo wake wa kwanza anga za kimataifa akikamilisha dakika zote 90 bila kutunguliwa.

US Monastir ushindi wao wa mabao 2-1 Real Bamako unawafanya wabaki nafasi ya pili wakiwa na pointi zao 13 tofauti ya mabao ya kufunga na kufungana na Yanga.

Timu hiyo imeandika rekodi tamu ya kushinda nje ndani dhidi ya TP Mazembe kwenye hatua ya makundi katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa ilishinda mabao 3-1 na jana ikashinda bao 0-1.

Previous articleKINZUMBI ATAJA SABABU ZA KUSAINI YANGA, MGUNDA AACHIWA MSALA
Next articleAZAM FC KWENYE KAZI LEO NA MTIBWA SUGAR