WAKONGWE WAMEGOMEA KUSTAAFU, WANAPIGA KAZI

MCHEZO wa soka la kisasa unakua kwa kasi na wanasoka wanaonekana kuwa wachanga kila wakati, lakini bado kuna nafasi kwa wahenga kuendelea kuchangia uzoefu wao.

Pamoja na maendeleo ya mara kwa mara katika teknolojia na lishe, sasa imekuwa kawaida kwa wanasoka kucheza hadi mwisho wa miaka thelathini na hata hadi arobaini.

Hapa kuna wachezaji ambazo hawezi kuamini kuwa bado wanaendelea kukipiga msimu huu. Kuna baadhi ya majina ya kufurahisha katika hili.

Roque Santa Cruz

Mshambuliaji huyu wa zamani wa Blackburn Rovers bado anajua goli lilipo akiwa na miaka 41 sasa. Tangu 2016 amekuwa akicheza nchini Paraguay, ambapo amefunga mabao 75 katika mechi 178.

Alifanya uhamisho wenye utata kutoka Club Olimpia kwenda kwa wapinzani wao, Club Libertad Januari. Hatua hiyo ilimfanya kupoteza maelfu ya wafuasi kwenye mitandao ya kijamii.

Phil Jagielka

Baada ya kucheza kwa muda mfupi Sheffield United na Derby County, Jagielka amepata kazi yake mpya huko Stoke City.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 41, hivi karibuni alicheza mechi yake ya 600 kwenye ligi kwa kufunga bao dhidi ya Huddersfield Town.

Diego Godin

Mmoja kati ya mabeki wakali kucheza soka Ulaya, Godin ambaye ana miaka 37 kwa sasa anacheza Ligi Kuu ya Argentina katika kikosi cha Velez Sarsfield.

Alex Song

Song aligonga vichwa vya habari mwaka jana alipofichua sababu ya yeye kuondoka Arsenal na kwenda Barcelona mwaka 2012.

“Nilikutana na mkurugenzi wa michezo wa Barca,” Song alisema kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram, “Na akaniambia sitaweza kucheza michezo mingi, lakini sikujitolea – nilijua kuwa sasa ningekuwa milionea.”

Pesa haiwezi kuwa motisha yake pekee, kwani Song mwenye miaka 35 bado anacheza soka kwa mabingwa wa Djibouti, Arta Solar 7.

Nani

Winga huyo wa Ureno alikuwa kati ya wachezaji wazuri pale Old Trafford. Sasa ana miaka 36, anacheza huko Australia katika kikosi cha Melbourne.

Claudio Bravo

Muda wa Bravo katika Manchester City ulikuwa wa kufurahisha sana. Kipa huyo wa zamani wa Barcelona alikuwa mmoja wa wachezaji wa kwanza kusajiliwa na Pep Guardiola akiwa City akichukua nafasi ya Joe Hart.

Sasa ana umri wa miaka 39, kipa huyo wa Chile ndiye chaguo mbadala katika Real Betis, akicheza nafasi ya pili nyuma ya Rui Silva.

Gael Clichy

Beki huyo wa pembeni wa Ufaransa alishinda mataji matatu ya Premier wakati akiwa na Arsenal na Man City na sasa anachezea Servette FC katika Ligi Kuu ya Uswisi akiwa na umri wa miaka 37.

Papiss Cisse

Msimu wa 2011-12 utaishi kwa muda mrefu katika kumbukumbu kwa mashabiki wa Newcastle kwani Cisse na Demba Ba walitengeneza pacha bora ambayo ilifananishwa kama ile ya Dwight Yorke na Andy Cole kwa msimu mmoja.

Baada ya kucheza nchini China na Uturuki, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 sasa anacheza Ligi ya Daraja la Pili ya Ufaransa katika klabu ya Amiens. Hatutachoka kutazama bao lake alilofunga dhidi ya Chelsea wakati akiwa Necastle.

Brad Jones

Kipa huyu raia wa Australia aliichezea Liverpool mechi 27 pekee katika kipindi chote cha miaka mitano aliyokaa klabuni hapo. Alikuja kupata zaidi nafasi ya kucheza baada ya kufikisha miaka 30 kuliko ilivyokuwa awali. Kwa sasa ana miaka 40.

Alicheza zaidi ya mechi 100 akiwa na Al-Nassr kwenye Ligi ya Saudia na sasa amerejea katika nchi yake ya asili ya Australia akiichezea Perth Glory.

Lukas Podolski

Podolski alicheza mechi yake ya kwanza kwa Ujerumani akiwa kijana na sasa bado anacheza akiwa na umri wa miaka 37. Alikaa miaka michache Vissel Kobe akiwa na Andres Iniesta na sasa anachezea miamba ya Poland, Gornik Zabrze.

Fabio Quagliarella

Kutoka kwa Antonio Di Natale hadi Francesco Totti, Serie A inaonekana kuwa mahali pa washambuliaji wakongwe kuwika.

Quagliarella ana miaka 40, ingawa nguvu zake zinafifia, bado anasubiri bao lake la kwanza la Serie A msimu huu. Kusema kweli, mechi nyingi alizocheza msimu huu amekuwa akitokea benchi pale Sampdoria ambapo timu iko kwenye hali mbaya katika msimamo.