>

MASTAA AZAM FC WAREJEA WAANZA KAZI

MASTAA wa Azam FC waliokuwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars wamerejea kambini na kuanza mazoezi na wachezaji wengine.

Nyota wawili wa Azam walikuwa kwenye kikosi cha Stars ambacho kilikuwa na kazi ya kusaka pointi sita dhidi ya Uganda kuwania kufuzu Afcon 2023.

Ni Abdul Suleiman, ‘Sopu’ na Nahodha msaidizi, Sospeter Bajana hawa walikuwa kwenye majukumu ya kupeperusha bendera ya Tanzania.

Haikuwa bahati kwenye mchezo wa pili uliochezwa Uwaja wa Mkapa walishuhudia ubao ukisoma Tanzania 0-1 Uganda lakini ule uliochezwa nchini Misri ubao ulisoma Uganda 0-1 Tanzania.

Mtupiaji wa bao alikuwa Simon Msuva ambaye alitumia pasi ya Dickson Job.

Mchezo ujao kwa Azam FC ni dhidi ya Mtibwa Sugar ambao ni wa robo fainali Kombe la Azam Sports Federation.