>

YANGA YAZIFUATA POINTI TATU DR CONGO

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe ambao ni wa hatua ya makundi kikubwa wanachohitaji ni pointi tatu.

Timu hiyo inakumbuka kwamba mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 hivyo wanakwenda ugenini kulinda ushindi na kusaka rekodi mpya wakiwa wanaongoza kundi na pointi 10.

 Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema kuwa wanatambua mchezo huo utakuwa mgumu lakini wanahitaji pointi tatu.

“Tuna mchezo dhidi ya TP Mazembe tunakumbuka tulipocheza nao hapa tulishinda na sasa tunawafuata tukiwa na ari ileile ya kusaka ushindi na kupata pointi tatu muhimu.

“Mashabiki tunatambua umuhimu wao na kuja kwao kutaongeza nguvu ndio maana tumewapa fursa ya kwenda kuiona timu yao ikitoa burudani na shangwe la kimataifa linahamia ugenini,” amesema.

Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi leo Machi 30 imeanza safari kuelekea DR Congo kwa ajili ya maadalizi ya mwisho ya mchezo huo wa mwisho hatua za makundi.

Miongoni mwa wachezaji ambao wapo kwenye msafara ni Dickson Job,Clement Mzize,Djuma Shaban,Jesus Moloko, Mudhathir Yahya, Bacca, Nkane Dennis.