>

MASTAA HAWA WANAWANIA TUZO, CHAMA NA MANULA VITA

MASTAA watatu wa Simba wamepenya kwenye msako wa kuwania tuzo ya mchezo bora wa mwezi.

Ni Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month) kwa mwezi Machi, 2023.

Wachezaji hao ni Jean Baleke wa DR Congo, Clatous Chama wa Zambia na Aishi Manula wa Tanzania.

Tuzo hiyo anayepewa chapuo ya kusepa nayo ni Chama huku akipewa upinzani mkubwa kutoka kwa Air Manula.

Air Manula kwenye mechi tatu mfululizo za Ligi ya Mabingwa Afrika hajaokota bao kwenye nyavu huku Chama akiwa amejaza kimiani mabao manne kwenye mechi hizo za kimataifa na Simba imetinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.