JESUS MOLOKO MIKONONI MWA MABOSI YANGA

MIONGONI mwa nyota ambao wanatajwa kuongezewa kandarasi ndani ya kikosi cha Yanga ni winga teleza Jesus Moloko.

Nyota huyo mkataba wake unatarajiwa kugota mwisho mwa msimu huu jambo amalo limewafanya mabosi wa Yanga kuanza mazungumzo naye.

Moloko inatajwa kuwa hakuongezewa mkataba kwa mpango kazi maalumu kisha wakamleta Tuisila Kisinda ambaye hajaonyesha ubora wake.

“Moloko hakupewa mkataba kwa mpango kazi maalumu na alipoletwa Kisinda ilikuwa ni mtego kwa wachezaji wote kuonyesha ujuzi.

“Kwa sasa hatua ambayo imefika sio mbaya anatarajiwa kuongeza mkataba mwingine kuendelea kuitumikia timu ya Wananchi,” ilieleza taarifa hiyo.

Moloko ndani ya ligi ametupia mabao matatu na ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.