AZAM FC KAZI INAENDELEA

BAADA ya ushindi kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC mpango kazi kwa Azam FC ni mchezo wao wa Azam Sports Federation hatua ya robo fainali.

Timu hiyo iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya KMC kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex ilikuwa Machi 27.

Kete yake inayofuata kwenye mechi za mashindano ni dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo wa hatua ya robo fainali.

Ofisa Habari wa Azam FC,Hasheem Ibwe amesema kuwa kila kitu kipo vizuri.

“Tupo vizuri na maandalizi yaaendelea kwa ajili ya mechi ambazo zipo na tunatambua kwamba ushindani ni mkubwa nasi tutafanya kazi kupata matokeo chanya,”.