MSAFARA WA SIMBA WAKWAMA KUWAFUATA RAJA

MSAFARA wa Simba ambao leo ulianza safari kueleke Morocco kupitia Qatar utaendelea na safari yake kesho Machi 29 2023 baada ya Ndege ambayo walianza nayo safari kupata hitilafu.

Hivyo mpango wa kuendelea na safari leo kuelekea Morocco umekwama mpaka siku ya kesho mapema baada ya maboresho ya chombo hicho cha usafiri.

Kwa mujibu wa Meneja wa Habari na Mawasiliano, Simba, Ahmed Ally amesema kuwa kikosi hicho kitapumzika Arusha kabla ya kuendelea na safari kuelekea Morocco.

Simba inatarajiwa kucheza na Raja Casablanca kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika unaotarajiwa kuchezwa usiku wa kuamkia Aprili Mosi ikiwa imeshatinga hatua ya robo fainali.