AFCON 2023:TANZANIA 0-0 UGANDA

UWAJA wa Mkapa mchezo wa kuwania kufuzu Afcon 2023 Ivory Coast ngoma bado ni nzito kwa pande zote.

Ubao unasoma Tanzania 0-0 Uganda ambapo kila timu inafanya mashambulizi kwa wapinzani kupata ushindi.

Tanzania inamtumia Simon Msuva, Mbwana Samatta pamoja na Sopu kwenye upande wa ushambuliaji huku Uganda wakiwa na Emmanuel Okwi na Khalid Lwaliwa ambao wanasumbue eneo la ushambuliaji.