UPENDO ni bora zaidi kwenye ulimwengu wa mpira kwa kuwa unatuunganisha pamoja popote ambapo tupo na hivyo ni muhimu kwa wale ambao wanacheza kuwa makini.
Muda huu kuna baadhi ya wachezaji wapo kwenye mapumziko kutokana na timu za taifa kuwa na kazi kwenye kuwania tiketi ya kufuzu Afcon.
Hii ipo wazi lakini wapo wachezaji ambao wapo kwenye kambi za timu za taifa kwa ajili ya mechi ambazo zinatarajiwa kuchezwa kwenye hili nalo ni muhimu kuzingatia.
Kwa wachezaji ambao wapo kwenye timu za taifa ni muhimu kukamilisha majukumu yao kwa umakini kwenye kusaka ushindi ndani ya uwanja.
Hii itakuwa fursa kwao kuonyesha ulimwengu kwamba wakiwa kwenye majukumu ya taifa wanatimiza kazi kwa umakini na kuwapa furaha mashabiki.
Sio kuwapa mashabiki furaha tu bali hata thamani yao kwenye soko inakuwa hapo watakuwa wanafanya kazi moja kwa wakati mmoja jambo ambalo ni kubwa
Wale ambao watazembea fursa hii wana kazi ya kujipanga wa wakati ujao kwani wanaweza wasiitwe kwenye timu hizo jambo litakalowapa maumivu.
Ukweli ni kwamba yule anayefanya vizuri kwenye timu ya taifa anazidi kuongeza thamani yake mwenyewe pamoja na kuongeza thamani ya nafasi ya timu ya taifa.
Nina amini kwamba kila mchezaji anapenda kuona timu inapata matokeo basi iwe ni kwa vitendo kwenye kutafuta ushindi na kuwapa furaha mashabiki.
Kwa mashabiki ni muda wa kuendelea kuwa bega kwa bega na timu kwenye mashindano ambayo wanashiriki hasa kwa kujitokeza uwanjani katika mechi za nyumbani.
Uwepo wenu uwanjani una nguvu na unafanya kila mchezai kuona ana deni kukamilisha majukumu yake awapo uwanjani kwa kusaka ushindi.
Ukiweka kando suala la majukumu ya tim ya taifa kuna Ligi Kuu Bara ambayo kwa sasa ipo kwenye lala salama ni muhimu kila mchezaji kulijua hilo.
Tunatambua kwamba wachezaji mnatambua lakini kwenye umaliziaji wake kumekuwa na matumizi makubwa ya nguvu jambo ambalo sio sawa.
Huu ni muda wa kutumia akili kubwa kwenye kusaka matokeo na kulindana hasa ukizingatia msimu unakaribia kugota mwisho.
Ikiwa msimu unagota mwisho kisha mchezaji akaumizwa na mchezaji mwenzake inaumiza unajua hasa muda ambao atautumia kuwa nje ya uwanja.
Kikubwa ni kuheshimu mpinzani na kucheza kwa umakini kwenye msako wa poiti tatu nah ii itafanya ligi izidi kuwa na ushindani pamoja na mvuto kuongezeka.
Ile ligi ya kukatana mabuti na kuumizana kabisa haipendezi kwa kuwa inarudisha nyuma maendeleo ya mchezaji binafsi pamoja na timu.
Mchezaji anapofanyiwa usajili mpango mkubwa kwa timu ni kupata huduma yake pale wanapokosa nafasi ya kumtumia kisha akawa anatumia muda mwingi nje ya uwanja hii haipendezi.
Haipendezi kuona mchezaji tegemeo anatumia muda mwingi kutokana na kuumziwa na rafiki yake uwanjani hili lisipewe nafasi na badala yake uungwana utumike kwenye kila mechi.
Kushuka kupo na bingwa atapatikana ndani ya ligi lakini kuumizana sio jambo zuri kwenye mechi ambazo zimebaki ndani ya ligi.