Home Sports UGANDA WAIPIGA MKWARA HUU TANZANIA

UGANDA WAIPIGA MKWARA HUU TANZANIA

NAHODHA wa timu ya Taifa ya Uganda, Emanuel Okwi ameweka wazi kuwa kesho watapambana kupata matokeo dhidi ya Tanzania.

Uganda ipo Bongo ikiwa na kibarua cha kusaka ushindi dhidi ya Stars kwenye mchezo wa kuwania kufuzu Afcon 2023 Ivory Coast.

Katika mchezo uliochezwa Misri, ubao ulisoma Uganda 0-1 Tanzania huku bao likifungwa na Simon Msuva.

Kesho Machi 28 mchezo wa pili unatarajiwa kuchezwa ikiwa ni hatua ya makundi ambapo Okwi amesema wapo tayari kwa mchezo huo.

“Tumepoteza mchezo wa kwanza tukiwa nyumbani na sasa tumekuja hapa Tanzania tunajua mchezo utakuwa mgumu lakini tutapambana kupata matokeo mazuri

“Ukweli ni kwamba kila mchezaji yupo tayari kwa ajili ya kuona tunashinda na tutajitahidi kufanya vizuri kwenye mchezo wetu wa kesho,”.

Previous articleVIDEO:JAMBO LA NCHI,UTAPENDA AHMED/KAMWE NDIMBO BALAA
Next articleNABI AINGIZA WINGA MALI,STARS TAYARI KUIKABILI UGANDA