WAMEVUJA JASHO KINOMANOMA

STAA wa Manchester United, Bruno Fernandes ametumia dakika nyingi zaidi uwanjani kuliko mchezaji mwingine yeyote barani Ulaya msimu huu.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 amecheza asilimia 92 ya dakika zote ambazo Kocha Erik ten Hag amewaongoza Mashetani msimu huu na alianza mechi zote isipokuwa tatu kati ya 45 za mashindano yote.

Kama ilivyokuwa kwa Liverpool msimu uliopita, United wanasalia katika kila shindano wanaloshindana na wanaweza kumaliza msimu kwa kucheza idadi kubwa zaidi ya mechi.

Sio tu kwamba Bruno amecheza vyema katika klabu yake msimu huu, lakini pia alicheza zaidi ya dakika 500 kwenye kikosi cha Ureno, ikiwa ni pamoja na mechi nne katika Kombe la Dunia huko Qatar mwaka jana.

“Bruno anaweza kukabiliana kwa viwango vya juu na anaweza kucheza mechi nyingi,” Ten Hag alisema kuhusu uamuzi wake wa kutompumzisha staa huyo zaidi msimu huu na kuongeza:

“Ni mchezaji ambaye yuko fiti na muhimu sana kwenye timu hii. Kwanza kama nahodha, yeye ni mfano uwanjani kwa nguvu anazoonyesha. Ni mfano mzuri kwa kila mtu kikosini.”

Bruno akimshinda mchezaji mwenzake wa Manchester United, David de Gea kama mchezaji aliyecheza dakika nyingi zaidi Ulaya msimu huu, huku makipa wenzake Alexander Nubel, Rui Patricio, Alex Remiro na Gianluigi Donnarumma wakiwa nusu ya 10 bora.

De Gea amecheza kila dakika ya mechi za United kwenye Premier League hadi sasa. Ndivyo ilivyo kwa Jordan Pickford, James Tarkowski, Illan Meslier, Gavin Bazunu, Gabriel Magalhaes, Jose Sa, Max Kilman, Aaron Ramsdale, Ederson, James Ward-Prowse, David Raya, Declan Rice na Danny Ward.

Kwingineko, wachezaji wawili wa Real Madrid, Vinicius Junior na Federico Valverde wanashika nafasi ya tatu na ya kumi, huku Mohamed Salah wa Liverpool akishika nafasi ya tisa.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa alikuwa na mapumziko ya katikati ya msimu baada ya Misri kushindwa kufuzu Kombe la Dunia Qatar 2022, ambayo inaweza kuwa msaada zaidi kutokana na kutumia maelfu ya dakika kwa klabu na nchi msimu uliopita.

Hapa kuna orodha ya wachezaji wachezaji 10 ambao wametumika kwa dakika nyingi zaidi barani Ulaya msimu huu. Takwimu ni kabla ya mechi za wikiendi iliyopita.

  1. Bruno Fernandes (Man Utd) – 3,751

  2. David de Gea (Man Utd) – 3,690

  3. Vinicius Junior (Real Madrid) – 3,510

  4. Axel Disasi (Monaco) – 3390

  5. Alexander Nubel (Monaco) – 3390

  6. Rui Patricio (Roma) – 3330

  7. Alex Remiro (Real Sociedad) – 3330

  8. Gianluigi Donnarumma (PSG) – 3330

  9. Mohamed Salah (Liverpool) – 3318

  10. Federico Valverde (Real Madrid) – 3314