WAWILI WAONGEZWA STARS

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania, Wallace Karia amesema wachezaji wawili wazoefu kwenye timu ya Taifa ya Tanzania Shomari Kapombe na Mohamed Hussein wameongezwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania.

Hiyo ikiwa ni baada ya timu ya Stars kukamilisha mchezo wa kwanza ugenini dhidi ya Uganda na kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Tayari kikosi cha Stars kimerejea Dar kikitokea Misri kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa pili dhidi ya Uganda unaotarajiwa kuchezwa uwanja wa Mkapa Jumanne.

Karia amesema wachezaji hao wameongezwa na kocha mwenyewe ambaye aliwachagua wachezaji wale wa awali walioingia kambini mapema.

“Kocha amewaongeza wachezaji wawili kambini ambao ni Mohamed Hussein na Shomari Kapombe kwa ajili ya mchezo dhidi ya Uganda na ni yeye mwenyewe amewaona na kuwaongeza kwenye kikosi,”.