>

MKWANJA WA SIMBA KUTUMIKA KWA UMAKINI

MWENYEKITI wa Bodi ya Simba, Salim Muhene amesema kuwa  udhamini ambao wamepata kwa timu ya vijana wenye thamani ya milioni 500 ni mkubwa na watatumia fedha hizo kwa umakini mkubwa.

Machi 23Klabu ya Simba iliingia mkataba wenye thamani hiyo na Kampuni ya Mobiad Afrika katika Hotel ya Serena na viongozi wa pande zote mbili walikuwepo.

 Ni mkataba kwa ajili ya kudhamini soka la Vijana la timu hiyo, ‘Simba Youth’ ili kuendeleza vipaji vya wachezaji vijana.

Kiongozi huyo amesema:“Jambo hili lina neema kubwa. Niwashukuru MobiAd kwa kukubali kudhamini timu yetu ya vijana. Kama Simba Sports Club tunawaahidi kwamba fedha hizi zitatumika vizuri kwani vijana ndio msingi wa timu yetu,”.

Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajuna amesema kuwa kwa mkataba huo Simba inakwenda mbele katika kutambua na kuibua vipaji vya vijana.

Moabid kupitia kwa Norbert Leon ambaye ni Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Moabid Afrika amesema:”Simba nawapongeza kwa kuwa na huu mpango ambao utawasaidia huko mbeleni. Hatutaki kwenye timu siku akina Bocco wakiondoka pale timu inapata matatizo,”