JASHO LA HAKI KWA SIMBA NA HOROYA LILIVUJA NAMNA HII

JASHO la haki liliwavuja wachezaji wa timu zote mbili ndani ya dakika 90 kusaka ushindi na mwisho wababe wakawa ni Simba.

Ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 7-0 Horoya huku wawakilishi hao wakitinga hatua ya robo fainali ilikuwa ni Machi 18,2023 na kazi ilikuwa namna hii:-

Aishi Manula

Alipiga pasi ndefu dakika ya 2,27,38,41,64,65,73,79,80 alipiga pasi fupi dakika ya 3,37,41,58,68, aliokoa dakika ya 14,38,64,65,72,74.

Henock Inonga

Beki huyu alikuwa na kazi kubwa kuokoa mashambulizi ya wapinzani wake ambapo aliokoa dakika 3,10,21,14,45,64,79,80 alichezewa faulo dakika ya 13 alimwaga krosi dakika ya 15.

Kanoute

Kamba mbili alitupia nyavuni kwa mashuti akiwa nje ya 18 akitumia mguu wake wa kulia ilikuwa dakika ya 54 na 87 aliokoa hatari dakika ya kwanza, 23,41,45,47,56 alicheza faulo dakika ya 40.

Zimbwe Jr

Mohamed Hussein Zimbwe Jr aliokoa dakika ya kwanza, 15,26,43,46.

Chama

Kama tatu alitupia kwenye mchezo dhidi ya Horoya ilikuwa dakika ya 10,36 na 70 ambapo alisepa na mpira wake huku akiokoa hatari dakika ya 67,81 alirusha dakika ya 43 alicheza faulo dakika ya 18 zile krosi alimwaga dakika ya 11,17,45,58.

Kapombe

Shomary Kapombe alimwaga krosi dakika ya kwanza,4,31,45,77,80 alisababisha penalti dakika ya 31, aliokoa hatari dakika ya 3,4,47,51.

Onyango

Joash Onyango aliokoa hatari dakika ya kwanza, 4,10,13,26,38,41,45,55,90 alicheza faulo dakika ya 37

Jean Baleke

Baleke kwenye eneo la ushambuliaji alianza akifunga mabao mawili dakika ya 32,65 alichezewa faulo dakika ya 29 alipiga mashuti ambayo yalilenga lango dakika ya 47 pamoja na 36,65 alichezewa faulo dakika ya 8,51.Aliyeyusha dakika 81 nafasi yake ilichukuliwa na Moses Phiri.

Kibu Dennis

Alipiga mashuti ambayo yalilenga lango dakika ya 30,54 alicheza faulo dakika ya 4,29,36,41 pia alionyeshwa kadi ya njano aliyeyusha dakika 56 nafasi yake ilichukuliwa na Pape Sakho ambaye alicheza faulo dakika ya 59 na kuonyeshwa kadi ya njano.

Mzamiru

Mzamiru Yassin alionyeshwa kadi moja ya njano kwenye mchezo ambapo alicheza faulo dakika ya 28,39 aliyeyusha dakika 81 nafasi yake ikawa mikononi mwa Erasto Nyoni.

Ntibanzokiza

Saido Ntibanzokiza alipiga kona dakika ya 3,47,48, alimwaga krosi dakika ya 3,5,13 alipiga mashuti ambayo hayakulenga lango dakika ya 15,17 na alikutwa kwenye mtego wa kuotea dakika ya 49.

Hawa hapa ni Horoya kazi yao ilikuwa namna hii:-

Mussa Kamara

Alianza langoni kipidi cha kwanza akiyeyusha dakika 45 ambapo alitunguliwa mabao matatu ilikuwa dakika ya 10,32 na 36 kwa mkwaju wa penalti ambapo alipiga mipira mirefu dakika ya 5,45.

Ni Sekou Sylla alichukua nafasi ya Kamara langoni yeye alitunguliwa mabao manne dakika ya 54,65,70,87.

Salif Coulibary

Jitu hili lililokwenda hewani lilikutana na kazi nzio Uwanja wa Mkapa kwenye eneo la ulinzi licha ya kufanya kazi kubwa bado aliokota nyavuni mabao 7.

Aliokoa hatari dakika ya 18,21,24,25,30,36,37,44,53,55,59 alicheza faulo dakika ya 4,50 alipiga faulo dakika 25,28,39.

Ismail Samake

Ni kazi ya kurusha alifanya dakika ya 14,26 alimwaga krosi dakika ya 18,24,26,37,45 alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 45.

Fofana

Mohamed Fofana aliokoa hatari dakika ya 58,64,73,80 kwenye mchezo huo.

Ndiaye

Pape Ndiaye aliyewafunga bao Simba kwenye mchezo ule uliopita alikuwa kwenye kazi nyingine dakika ya 20 alikutwa kwenye mtego wa kuotea alipiga mashuti ambayo hayakulenga lango dakika ya 26,37.

Na Dizo Click imetoka gazeti la Championi Jumatatu.