Home Sports AZAM FC REKODI ZA NYOTA WAO ZINASOMA HIVI

AZAM FC REKODI ZA NYOTA WAO ZINASOMA HIVI

KUNA vingi vya kujivunia kwenye ardhi ya Tanzania ikiwa ni pamoja na mlima Kilimanjaro kutokana na kuwa na kilele chenye ubora.

Kwenye ulimwengu wa soka kuna maskani ya Azam FC yalipo maskani ya timu bora ambayo inapambana kuonyesha ubora kwa vitendo, hapa tupo nao kwenye mwendo wa data kutazama kazi zao namna hii:-

Mechi nyingi

Daniel Amoah

Kitasa cha kazi kikiwa kimeanza kikosi cha kwanza kwenye mechi nyingi kuliko wachezaji wote ambazo ni 22 kwenye ligi pekee.

Beki huyo ana uwezo wa kuzuia mashambulizi na kufunga akiwa ametupia mabao mawili na yote ni kwa mapigo ya vichwa akitumia pasi za Ayoub Lyanga.

Timu yake ya kwanza kuitungua ilikuwa Yanga kisha ikafuata Mtibwa Sugar, Uwanja wa Manungu.

Pasi za mwisho

Ayoub Lyanga huyu ni mtaalamu wa kazi hizi za kutengeneza mipango ndani ya Azam FC akiwa ametengeneza pasi saba.

Mzuri kwenye mapigo huru akiwa amemtengenezea pasi mbili mshikaji wake Amoah zote kwa mtindo huo ndani ya ligi.

Kiungo huyu ameanza kikosi cha kwanza mechi 13 na ametupia kambani mabao mawili bao lake la kwanza ilikuwa dhidi ya Polisi Tanzania.

Ngumi jiwe

Mwamba Malickou Ndoye anaingia kwenye mtego huu akiwa ni nyota aliyeonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kutokana na kitendo chake cha kuonekana akimpiga kiwiko nyota wa Dodoma Jiji, Justin Billary ilikuwa dakika ya 44.

Hiyo ilikuwa ni Februari 4,2022 ubao wa Uwanja wa Jamhuri, Dododoma ulisoma Dodoma Jiji 2-1 Azam FC.

Mkali akitokea benchi

Desemba 15,2022 Kagera Sugar 2-2 Azam FC, alitokea benchi akafunga na kutoa pasi ya bao kwenye mchezo huo.

Novemba 27, ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Azam FC 3-2 Coastal Union alitokea benchi akafunga na kutoa pasi ya bao.

Ni yeye anaitwa Idd Suleiman, ‘Nado’ akiwa ameanza kikosi cha kwanza mechi nne pekee huku kibindoni akiwa na mabao manne na pasi mbili za mabao ambazo zote alizotoa akitokea benchi.

Zuber Foba

Kipa namba nne wa Azam FC mchezo wake wa kwanza kupewa nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza alitunguliwa bao moja ndani ya dakika 90.

Ilikuwa ni Septemba 30,2022 ubao wa Sokoine ulisoma Tanzania Prisons 1-0 Azam FC na kuifanya miamba hiyo kuyeyusha pointi tatu mazima.

Mtambo wa mabao

Ni Idris Mbombo nyota huyu hajawa kwenye mwendelezo bomba kutokana na kutokuwa fiti mara kwa mara.

Kambani katupia mabao 7 ikiwa ni sawa na idadi ya mechi ambazo ameanza kikosi cha kwanza msimu huu ndani ta Azam FC.

Mbaya wa Simba

Prince Dube kawatungua Simba mabao mawili kwenye mechi zote mbili ndani ya dakika 180 ikiwa ni pamoja na lile bao la mapema zaidi sekundi ya 15.

Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza bao lake lilidumu mpaka dakika ya 90 Azam FC wakasepa na pointi tatu mazima ule wa pili ngoma ilikuwa 1-1.

Imeandikwa na Dizo Click imetoka gazeti la Championi Jumatatu, Machi 20 2023.

 

Previous articleVIDEO:YANGA HAWANA HOFU KIMATAIFA,KAZI INAENDELEA
Next articleJASHO LA HAKI KWA SIMBA NA HOROYA LILIVUJA NAMNA HII