Home Uncategorized IHEFU WANA BALAA HAO

IHEFU WANA BALAA HAO

WABABE kutoka Mbeya, Ihefu wakiwa Uwanja wa Highland Estate wanabalaa dhidi ya vigogo ambao walikutana nao katika uwanja huo.

Yanga bado wanakumbuka namna walivyotunguliwa kwenye ligi kwa msimu wa 2022/23 walipotua ndani ya uwanja huo.

Ubao wa Uwanja wa Highland Estate ulisoma Ihefu 2-1 Yanga na kutibua ie rekodi ya kutaka kufikisha mechi 50 bila kufungwa za ligi na kugotea namba 49.

Azam FC ndoto zao za kutwaa ubingwa zimekomea palepale Highland Estate baada ya ubao kusoma Ihefu 1-0 Azam FC.

Timu hiyo yenye maskani yake Mbeya ilianza msimu kwa kusuasua lakini kwa sasa imerejea kwenye reli ikiwa inashusha dozi kwa wapinzani wao.

Februari walisepa na tuzo mbili ikiwa ni mchezaji bora ambaye ni Yacouba Songne pamoja na meneja bora wa uwanja ambaye ni Malule Omary.

Previous articleWIKENDI HII TUSUA PESA UKIWA NA MERIDIANBET, VIWANJA MBALIMBALI KITAWAKA
Next articleTUNASEMAJEE MMEKUJA WAKATI MBAYA