KIMATAIFA MUHIMU KUUNGANA KUTUSUA

IKIWA watakuja wageni na kuondoka na ushindi nyumbani kweye hatua za makundi mechi za kimataifa ni maumivu makubwa kwelikweli.

Hiana maana kwamba waohawana uwezo wa kushinda lakini ni namna ya uhitaji ulivyo mkubwa kwa sasa kwa kila timu hasa Simba na Yanga.

Mechi za nyumbani kwa kila mmoja kwa sasa zimeshikilia maamuzi ambayo yataleta hatua kubwa kwenye soka letu la nyumbani hivyo ni muhimu wachezaji kupambana kupata ushindi.

Wale ambao wamekata tamaa kwenye mechi za nyumbani ni muhimu kupambana na kurejesha matumaini ili kupata ushindi.

Hakika sio kazi nyepesi kwa wawakilishi wa kimataifa ukizingatia kwamba kila mmoja ambaye anafanya kazi kubwa kwenye kusaka ushindi ni lazima ajitume.

Hakika wakati huu ni muhimu kufanya kazi kubwa kwa kuwa makini kwenye mechi za kimataifa ambazo zipo na kila mmoja ni muhimu kujituma.

Wachezaji wana kazi kubwa kwa sasa kufanya kazi ya kusaka ushindi  kwani dakika 90 za nyumbani ni dhahabu kwa kila mmoja.

Ikawe kazi nzuri kwa wachezaji kutimiza majukumu yao na inawezekana ukizingatia kwamba ni mechi zao ambazo watakuwa nyumbani.

Mashabiki wao uwanja wao na kila kitu kinawapa nafasi ya kushinda lakini wanapaswa kuwaheshimu wapinzani wao kwani nao wanahitaji matokeo.

Inwezekana kufanya kazi kubwa na nzuri na kufungua ukurasa mwingine kimataifa muda ni sasa na kila kitu kinawezekana huku nidhamu iwe kubwa kwa kila mmmoja.