DROO ya mashindano ya Azam Fedaration hatua ya robo fainali imechezeshwa leo Machi 15,2023 Dar, watani wa jadi Simba na Yanga hawatakutana katika hatua ya robo wala nusu fainali.
Msimu uliopita Yanga ilicheza nusu fainali dhidi ya Simba na kushinda 1-0 kisha ikatinga fainali ikamenyana na Coastal Union ya Tanga.
Robo fainali ilivyochezeshwa ngoma itakuwa namna hii:-
Simba vs Ihefu
Singida Big Stars vs Mbeya City
Yanga vs Geita Gold
Azam FC vs Mtibwa Sugar
Nusu fainali
Mshindi wa mchezo wa Simba vs Ihefu dhidi ya mshindi wa mchezo wa Azam vs Mtibwa Sugar
Mshindi mchezo wa Singida Big Stars dhidi ya mshindi wa mchezo kati ya Mbeya City dhidi ya Yanga vs Geita.
Mechi za nusu fainali zitachezwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara na Liti Singida
Fainali
Fainali ni CCM Mkwakwani Tanga.