YANGA YATEMBEZA BONGE LA MKWARA KWA WAARABU

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa maandalizi kuelekea mchezo wa kimataifa wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Monastir ya Tunisia yapo sawa.

Kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa ugenini nchini Tunisia Yanga ilipoteza kwa kushuhudia ubao ukisoma US Monastir 2-0 Yanga watakuwa na kazi ya kusaka ushindi Jumapili.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema waache Waarabu hao wa Tunisia waje Uwanja wa Mkapa wamalizane nao kwa kuwa wana deni nao.

”Maandalizi ya mchezo wa Jumapili yanaendelea vizuri na uongozi umeanza maandalizi ya kishindo kuelekea mchezo huu lipo tayari kwa ajili ya kupata ushindi kwenye mchezo huu wa kimataifa ambao ni muhimu.

“Ni mbinu nyingi ambazo zipo na benchi la ufundi jana mliona pale Chamazi baada ya wale Geita kutaka kutujaribu hawakuamini walichokiona hivyo mashabiki na wanachama mjitokeze kwa wingi na tumefunga kampeni rasmi kwa ajili ya mchezo wetu wa kimataifa,” amesema.

Tayari tiketi zimeanza kuuzwa kwa mashabiki na wanachama wote Tanzania.

Slogan ya mchezo huo wa kimataifa Yanga wanasema:’Full House, Full Shangwe..Waje Tumalizane.