FISTON Mayele mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Geita Gold.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex saa 1:00 usiku.
Ngoma inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu zote kusaka pointi tatu.
Mayele amesema:”Ni mchezo muhimu kwetu na tunahitaji kupata pointi tatu mashabiki wawe pamoja nasi.
“Tupo tayari kwa mchezo ambao utakuwa na ushindani mkubwa, Geita Gold dhidi yetu mchezo haujawahi kuwa rahisi hivyo tutajitahidi kusaka ushindi,”.