KMC YAVUNJA REKODI MBOVU YASHINDA KWA MARA YA KWANZA

KMC inayonolewa na Hitimana Thiery iliambulia pointi moja kwenye sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar huku mechi sita wakiambulia kichapo mazima.

Timu hiyo KMC ilishuhudia ubao ukisoma KMC 1-3 Simba, Desemba 26,2022,Ihefu 1-0 KMC, Januari 3,2023,Mtibwa Sugar 1-1 KMC, Januari 13,2023.

KMC 1-3 Namungo, Januari 24,2023,Ruvu Shooting 2-1 KMC, Februari 5,KMC 0-1 Yanga Februari 22 na Azam FC 1-0 KMC Februari 25.

Ushindi huo unaifanya ifikishe pointi 26 kibindoni baada ya kucheza mechi 25.

Huu unakuwa ni ushindi wa kwanza ndani ya 2023 kwa KMC.

Mtupiaji wa mabao Daruesh Saliboko amesema kuwa hawakuwa na mwendo mzuri ndani ya mwaka na kupata ushindi ni furaha kwao.

“Ilikuwa ni kazi kubwa kwetu licha ya kucheza vizuri kwenye mechi tulikuwa tunakosa matokeo na huu ni ushindi wetu wa kwanza tangu mwaka upinduke.

“Bado tutazidi kupambana kwenye mechi ambazo zimebaki ili kupata matokeo mazuri,”.