YANGA WALIWAKIMBIZA REAL BAMAKO KWA MKAPA

UKIWEKA kando Yanga kusepa na pointi tatu mazima dhidi ya Real Bamako walitawala katika kila Idara huku wakicheza Kwa tahadhari licha ya kuwa wapo nyumbani.

Mashuti waliyopiga ni 12 huku manne yakilenga lango na mawili yàkizama nyavuni watupiaji wakiwa ni Fiston Mayele dakika ya 8 na Jesus Moloko dakika ya 68.

Bamako ni mashuti 11 walipiga huku moja lililenga lango na kuokolewa na Djigui Diarra.

Walitembeza mikato mara 17 Sawa na Real Bamako.

Umiliki wa mpira ilikuwa ni asilimia 53 huku Bamako wakiwa na asilimia 47.

Nafasi ya pili kwenye kundi wakiwa na pointi 7 kibindoni huku vinara wakiwa ni US Monastir wenye pointi 10, TP Mazembe nafasi ya tatu pointi tatu na Real Bamako nafasi ya nne pointi mbili wakiwa kundi C la Kombe la Shirikisho Afrika.

Kituo kinachofuata kwa Yanga ni dhidi ya vinara wa kundi Monastri mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Machi 19,2023.

Pia baada ya mchezo kukamilika walikabidhiwa milioni 10 za mama ikiwa ni ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu.