YANGA YAITUNGUA REAL BAMAKO KIMATAIFA

BAADA ya Fiston Mayele kupachika bao la kuongoza kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya makundi msumari mwingine umejaa kimiani.

Ubao wa Uwanja wa Mkapa unasoma Yanga 2-0 Real Bamako ikiwa ni mchezo wa kimataifa.

Mayele alianza kupachika bao dakika ya 8 akiwa ndani ya 18 lilidumu mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili Mayele alisababisha penalti ambayo ilipigwa na Yannik Bangala ikaenda juu kabisa ya lango.

Jesus Moloko alipachika bao la pili dakia ya 68 kwenye mchezo huo ambao umehudhuriwa na mashabiki wengi.

Yanga inasepa na pointi tatu muhimu kwenye mchezo wa kimataifa hatua ya makundi.