TIZI LA MWISHO LA SIMBA LILIKUWA NOMA

KIKOSI cha Simba jana Machi 6,2023 kilifanya mazoezi ya mwisho Kwa ajili ya kuikabili Vipers mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni hatua ya makundi.

Simba ambayo ipo kundi C ikiwa na pointi tatu nafasi ya tatu Leo ina kibarua cha kusaka pointi nyingine Uwanja wa Mkapa Saa 1:00 usiku.

Katika mazoezi hayo wachezaji wote wa Simba walionekana kufuata maelekezo ya benchi la ufundi Kwa umakini huku wakiwa na morali ya hali ya juu Kwa ajili ya mchezo wa Leo.

Kocha Mkuu wa Simba, Robert Oliviera akishirikiana na Juma Mgunda walikuwa wakiwapa maelekezo vijana wao mbinu za kuikabili Vipers.

Miongoni mwa wachezaji waliokuwa katika mazoezi ni pamoja na Aishi Manula,Beno Kakolanya,Moses Phiri,Jean Baleke, Clatous Chama, Henock Inonga, Mzamiru Yassin,Pape Sakho,Shomari Kapombe,John Bocco,Sadio Kanoute,Ismail Sawadogo pamoja na Jonas Mkude.

Kiungo Kibu Dennis ambaye juzi alianza program maalumu peke yake kutokana na kutokuwa fiti Jana alianza mazoezi ya kawaida na wachezaji wenzake.

Wachezaji walianza na mazoezi ya utimamu wa mwili kisha baadaye mpango wa mbinu za kuimaliza Vipers zilifuata.

Ikumbukwe kwamba mchezo uliopita Simba ikiwa ugenini ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Vipers na leo ina kazi ya kusaka pointi tatu nyingine kufikisha pointi sita ambazo zitafufua matumaini timu hiyo kutinga robo fainali.