WIKI YATIMIA KWA MANCHESTER UNITED

LIVERPOOL hawakuwa na huruma kwenye mchezo wa Ligi Kuu England baada ya kushinda jumla ya mabao 7 huku wakisepa na pointi tatu mazima.

Ni Cody Gakpo alitupia kambani mabao mawili dakika ya 43 na 50, Darwin Nunez pia alitupia kambani mbili dakika ya 47 na 75.

Mohamed Salah alitupia mawili dakika ya 66 na 83 jioni Robert Firmino alitupia kambani dakika ya 88.

Yote haya yalifanyika Uwanja wa Anfield na sasa Liverpool imefikisha pointi 42 nafasi ya 5 huku United ikiwa nafasi ya tatu na pointi 49.