HIZI HAPA ZIMETINGA ROBO FAINALI AZAM SPORTS FEDERATION

AZAM FC imekamilisha idadi ya timu 8 ambazo zimetinga hatua ya robo fainali Azam Sports Federation.

Timu hiyo iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mapinduzi kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Mchezo huo wa hatua ya 16 bora ulikuwa ni wa mwisho kwa Machi 5 ambapo ule wa awali kabisa ulichezwa saa 10:00 jioni Uwanja wa Kaitaba.

Kwenye mchezo huo ubao ulisomaKagera Sugar 0-1 Mbeya City hivyo Mbeya City safari imeendelea mbele huku Kagera Sugar wakigota mwisho.

Mchezo huo pia ulishuhudia kadi nyekundu kwa kipa Chalamanda ambaye alimchezea faulo mchezaji wa Mbeya City kwenye harakati za kuokoa hatari.

Timu nyingine ni Yanga, Simba, Mbeya City, Geita Gold, Singida Big Stars, Ihefu SC, Mtibwa Sugar ambapo droo itaamua nani atakutana na nani