KILE chumba cha mafanikio kilichokuwa kina giza totoro mwanzo mwisho angalau sasa mwanga umeanza kupenya huku ile dhahabu ikianza kupata moto.
Ni wawakilishi wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika walifanikiwa kupata ushindi ugenini baada ya ubao kusoma Vipers 0-1 Simba, Februari 25,2023 Uwanja wa St Mary’s, hapa tunakuletea kazi ilivyokuwa namna hii:-
Aishi Manula
Hajaokota bao langoni kwa mara ya kwanza hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo aliokoa hatari dakika ya 3,11,28,35,47,61,65,77,82,88 huku akipewa jukumu la kupiga faulo dakika ya 50.
Alipiga mipira mirefu dakika ya 8,90 alichezewa faulo dakika ya 35,83.
Shomari Kapombe
Jukumu la kurusha lilikuwa kwenye mikono yake alifanya hivyo dakika ya 5,31,37,61,63,74,82 alicheza faulo dakika ya 59 alimwaga krosi dakika ya 16,63 alichezewa faulo dakika ya 28,50 aliokoa hatari dakika ya 39,49.
Henock Inonga
Nyota wa kwanza kufunga bao ndani ya Simba hatua ya makundi alifanya hivyo dakika ya 19, aliokoa hatari dakika ya 2,24,26,28,31,33,41 alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 53.
Joash Onyango
Beki chuma kwenye eneo lake la ulinzi aliokoa hatari dakika ya 6,12,24,46,58,59,66
Mohamed Hussein
Kwa upande wa Mohamed yeye alimwaga krosi dakika ya 62 huku akichezewa faulo dakika ya 33,alipiga faulo dakika ya 19, alirusha dakika ya 15,45 aliokoa hatari dakika ya 3,27,71.
Mzamiru Yassin
Kiungo wa kutibua mipango alivuja jasho huku akiokoa hatari dakika ya 30,46 alipiga shuti dakika ya 78 ambalo lililenga lango alicheza faulo dakika ya 23,51,90 huku akichezewa faulo dakika ya 26
Sadio Kanoute
Kazi ngumu zipo kwenye miguu yake alicheza faulo dakika ya 4 alichezewa faulo dakika ya 44 huku akiokoa hatari dakika ya 21,23,32.
Kibu Dennis
Rasta alianza kikosi cha kwanza alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 80 alipiga shuti lililolenga lango dakika ya 16 ambalo halikulenga lango ilikuwa dakika ya 40 alichezewa faulo dakika ya 17,72 aliyeyusha dakika 81 nafasi yake ilichukuliwa na Habib Kyombo ambaye alicheza faulo dakika ya 82
Ntibanzokiza
Saido Ntibanzokiza alipewa majukumu ya kupiga kona dakika ya 8,27,64 alichezewa faulo dakika ya 11,48,48 alirusha dakika ya 17,17,19 alicheza faulo dakika ya 40,58,65,69 na ni dakika ya 75 alipiga shuti ambalo lililenga lango.
Clatous Chama
Chama alipiga krosi dakika ya 55, alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 6 alipiga mashuti ambayo hayakulenga lango dakika ya 6,90 alicheza faulo dakika ya 32.
Moses Phiri
Ni pasi ya bao alitoa kwa Inonga dakika ya 19 alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 8 alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 40 alicheza faulo dakika ya 52 aliyeyusha dakika 60 nafasi yake ilichukuliwa na Erasto Nyoni ambaye aliokoa hatari dakika ya 69,89.
Vipers hawakuwa kinyonge kazi ilikuwa namna hii:-
Alfred Mudekeleza huyu alikuwa langoni alipookoa hatari dakika ya 75 huku akipiga pasi ndefu dakika ya 9,15,23,36.
Sentam Yunus
Nyota aliyefanya majaribio mengi kwa Manula ni huyu mwamba alipiga dakika ya 7,14,38,53,56 yote hayakulenga lango huku akikutwa kwenye wa kuotea dakika ya 14 na 53 alichezewa faulo dakika ya 53.
Hilaly Mukandara
Alikuwa kisiki kwenye kuokoa alifanya hivyo dakika ya 9,13,18,22 na 57 huku akipiga faulo dakika ya 69,90.
Asharaf Mandela
Mtaalamu kwenye kumwaga krosi za mbali ilikuwa dakika ya 45,46,71,83 aliokoa hatari dakika ya 17,40,45,72,87.
Milton Karisa
Kuumia kwa Karisa ilikuwa angalau kidogo kwa safu ya ulinzi kutokana na kasi ya mwamba kuliandama lango la Manula.
Alipiga krosi dakika ya 12,14,22 alicheza faulo dakika ya 35,39 shuti lililolenga lango dakika ya 35 na alikutwa kwenye mtego wa kuotea dakika ya 42 alipata maumivu dakika ya 44 nafasi yake ilichukuliwa na Ibrahim Orit.
Tambala Abdu
Aliokoa hatari dakika ya 22 alichezewa faulo dakika ya 23.
Martin Kiiza
Alicheza faulo dakika ya 50,82 alimwaga krosi dakika ya 54 na alichezewa faulo dakika ya 80,82.
Ikumbukwe kwamba kazi ya pili inatarajiwa kuchezwa Jumanne, Uwanja wa Mkapa huku sera ikiwa Jumanne ya Wenye Nchi.