ARSENAL WASEPA NA POINTI TATU KIBABE

LICHA ya Bournermouth kuanza kwa kasi kuliandama lango la Arsenal na kupata mabao ya kuongoza kila kipindi.

Bao la mapema lilifungwa dakika ya kwanza na Philip Billing na bao la pili lilifungwa na Marcus Senesi dakika ya 51.

Mwisho ubao ulisoma Arsenal 3-2 Bournemouth ambapo ni mabao ya Thomes Partey dakika ya 62, Ben White dakika ya 70 na bao la usiku la pointi lilifungwa na Reiss Nelson dakika ya 90+7.

Sasa Arsenal inafikisha pointi 63 ikiwa nafasi ya kwanza huku waliopoteza wakiwa nafasi ya 20 na pointi 21.

Meza imepinduliwa na pointi tatu zimesepa huku wageni hao kwenye mchezo wa leo wakikwama kusepa na pointi.