Home Sports SIMBA YATINGA ROBO FAINALI KWA 4G

SIMBA YATINGA ROBO FAINALI KWA 4G

MOHAMED Mussa nyota wa Simba amefunga bao lake la kwanza akiwa na Simba baada ya kujiunga na timu hiyo katika dirisha dogo dakika ya 69.

Ubao wa Uwanja wa Uhuru umesoma Simba 4-0 African Sports ikiwa ni mchezo wa hatua ya mtoano.

Bao la kwanza ni Mali ya Jean Baleke dakika ya 36, Kennedy Juma dakika ya 49 na kamba ya nne ni Jimsony Mwinuke alipachika bao hilo dakika ya 89 akitumia pasi ya Peter Banda.

Huu ni mchezo wa hatua ya 16 bora Kombe la Azam Sports Federation.

Previous articleSINZA MPO? MERIDIANBET IMEWALETEA DUKA LA KUBETIA NJOONI KWA WINGI MBASHIRI
Next articleVIDEO: SAKATA LA FEI TOTO LAMUIBUA MAMA