YANGA KUTUA DAR

MSAFARA wa kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi leo Februari 28 unatarajiwa kuwasili Dar.

Wawakilishi hao wa kimataifa kwenye anga la Kombe la Shirikisho walikuwa na mchezo wa hatua ya makundi dhidi ya Real Bamao uliochezwa Mali.

Kwenye mchezo huo ubao ulisoma Real Bamako 1-1 Yanga na kuwafanya wagawane pointi mojamoja kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Februari 27 kikosi kilianza safari kutoka Mali na Kikosi kiliwasili salama Ethiopia kisha wakapata muda wa kupumzika hapo na leo asubuhi wanaanza safari ya kurejea Dar es Salaam.

Ikumbukwe kuwa kwenye mchezo huo bao la Yanga lilifungwa na mshambuliaji wao Fiston Mayele akitumia pasi ya Aziz KI.

Ilikuwa ni Februari 26 walipotupa kete hiyo kwenye anga za kimataifa ugenini ikiwa kwenye kundi D na pointi zake ni nne.